Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkombozi wa mkulima fedha za mikopo ya benki ni vikundi

59349 Nmbpic

Fri, 24 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Benki ya NMB imetoa mkopo wa zaidi ya Sh500 Milioni kwa ajili ya kuviwezesha vikundi vya wakulima.

Meneja Mwandamizi wa NMB, Carol Nyangaro amesema wakulima hao wamepewa mkopo huo kwa sababu dhamana yao kubwa ni umoja waliojiunga.

Akizungumza katika Jukwaa la Fikra la Mwananchi linaloangalia sekta ya Kilimo leo Alhamisi Mei 23,2019 na kufanyika katika ukumbi wa Kisenga usiku huu,  Nyangaro amesema benki hiyo inatoa mikopo mbalimbali na ni rahisi kuwapatia wakulima wanapoungana.

“Kikundi hiki ni mfano tu, lakini Benki yetu hufanya kazi na wakulima, tunawakopesha pesa kwa ajili ya pembejeo, maandalizi ya mashamba na maeneo mengine,” amesema Nyangaro.

Amewataka wakulima kujiunga kwenye vikundi hivyo kwa sababu nje ya kuwa ni dhamana, vinaweza kuwasaidia katika kupata masoko ya mazao yao.

 

Habari zinazohusiana na hii

Chanzo: mwananchi.co.tz