Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkenda atembelea ujenzi wa kiwanda cha Mbolea Dodoma

Fcddd868175844e903062690443d7e00 Mkenda atembelea ujenzi wa kiwanda cha Mbolea Dodoma

Wed, 20 Oct 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

WAZIRI wa Kilimo, Profesa Adolf Mkenda, amekagua kiwanda cha FOMI mjini Dodoma na kuona kinavyofanya kazi ikiwa ni lengo la kuona uwezekano wa kiwanda hicho kama kinaweza kuuza mbolea yake Tanzania kwa bei nafuu kwa wakulima na kupatikana kwa wingi na kwa wakati.

Katika ziara hiyo Waziri Mkenda, pamoja na wataalamu mbalimbali aliombatana nao amesema kiwanda kama hicho ambacho kipo nchini Burundi kinazalisha Tani kati ya 120,000 mpaka Tani 150,000 kwa mwaka kulingana na soko la mbolea huku kikiwa kimeanza ujenzi wa kiwanda cha kisasa Jijini Dodoma nchini Tanzania ambapo kitapokamilika kitakuwa na uwezo wa kuzalisha Tani 600,000 za mbolea ambazo ni zaidi ya mahitaji ya mbolea nchini Tanzania ambayo ni kati ya Tani 400,000 mpaka Tani 500,000 kwa mwaka.

Amesema kuwa wakati serikali inaendelea na mkakati wa ujenzi wa kiwanda kikubwa cha mbolea Tanzania vilevile inaendelea na mkakati wa kuhakikisha kuwa inatafuta mbolea inayoweza kupatikana kwa wakati na kuwafikia wakulima kwa bei nafuu.

Waziri Mkenda amemuhakikishia Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda hicho Ntirampeba Simon, kuwa serikali ya Tanzania itakuwa bega kwa bega kuhakikisha kuwa ujenzi wa kiwanda hicho unakamilika kwa wakati uliokusudiwa.

“Wawekezaji wote wanaowekeza kwenye biashara ya Pembejeo Tanzania tunawahakikishia kuwa Tanzania ni nchi salama kwa uwekezaji hivyo wajitokeze kwa wingi kwa ajili ya kuwekeza” amesema

Kwa upande wake Waziri wa Mazingira, Kilimo na Uvuvi wa Burundi Dk Rurema Deo-Guide, amesema kuwa mazungumzo hayo yamekuja wakati muafaka kwani yameongeza wigo mpana zaidi kwa kubadilishana mawazo katika sekta ya kilimo.

Dk Rurema, amesisitiza kuwa katika muktadha wa kuongeza uzalishaji na tija katika mazao ya kilimo kuna mambo muhimu mawili ya kuzingatia ambayo ni maji, ardhi na mbolea na katika nchi ya Burundi sekta ya mbolea imeimarika na uzalishaji unatosheleza mahitaji ya wakulima,

Chanzo: www.habarileo.co.tz