Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkataba mradi mkubwa gesi asilia waiva

D8e733f7f1a0d911f3b260ac3b50dda6 Samia Suluhu Hassan

Sat, 4 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Tanzania, itatia saini makubaliano ya awali na kampuni za mafuta wiki ijayo, kujenga mradi wa gesi asilia (LNG) wenye thamani ya Sh trilioni 70 sawa na dola za Marekani bilioni 30.

Rais Samia Suluhu Hassan, aliwaambia Wahandisi na Wakandarasi Jumamosi mjini Dodoma: "Tutasaini mkataba wa LNG keshokutwa."

"Ninataka kuwahakikishia serikali itatoa kipaumbele maalumu kwa wakandarasi wa ndani kama sehemu ya local content (uwezeshaji wazawa)," alisema.

Rais alikuwa akizungumza katika simu wakati wa kongamano la moja kwa moja ambalo liliandaliwa kupongeza juhudi zake katika kuimarisha wakandarasi wa ndani.

"Tutaendelea kuunga mkono sekta hii na hasa wahandisi wa ndani na wakandarasi," aliongeza.

Tanzania ilianza tena mazungumzo ya mradi huo uliokuwa ukisubiriwa kwa muda mrefu mwaka jana.

Timu ya mazungumzo ilikuwa imesema mapema mwaka huu kwamba serikali inaweza kutia saini makubaliano hayo mwezi Mei. Pande hizo ni pamoja na kampuni tano za mafuta na gesi ambazo ni- Shell, Equinor, ExxonMobil, Pavilion na Ophir.

Kiwanda cha LNG kinatarajiwa kujengwa mkoani Lindi na tayari wananchi walishalipwa fidia kupisha mradi huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live