Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkataba biashara Afrika kuleta fursa

Mazao Mkataba biashara Afrika kuleta fursa

Tue, 29 Jun 2021 Chanzo: ippmedia.com

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula, aliyasema hayo jana alivyokutana na Katibu Mtendaji wa Eneo huru la Biashara la Afrika (AfCFTA), Wamkele Mene, aliyekuja nchini kwa ajili ya kujitambulisha na kufahamiana na uongozi mpya wa nchi.

Akizungumza baada ya kujitambulisha Katibu Mkuu huyo, alisema ameridhishwa na hatua zinazochukuliwa na serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan, jambo lililoongeza nafasi yake ya uongozi Afrika.

“Sekretarieti inavutiwa na uamuzi wa serikali kushiriki tena kuchukua jukumu la uongozi ambalo limehusishwa tangu enzi za Rais Julius Nyerere, lengo ni kuonana na uongozi wa Tanzania na kushawishi umuhimu wa nchi kujiunga,” alisema.

Alisema baaada ya ukoloni, bara sasa linafanya kazi kufungua na kuunganisha bara ili kuunda masoko na kuwezesha biashara na kwamba eneo hilo ni suluhisho la changamoto za maendeleo na kwamba Afrika ina uwezo wa kuiwezesha Afrika kukua kibiashara, kuboresha uchumi wa kiwango na kuanzisha soko jumuishi.

Naye Balozi Mulamula alisema mkataba huo ulisainiwa na nchi nyingine Machi mwaka 2018 na ulinza kutumika Mei 2019, na kwamba Tanzania haijachelewa kwa kuridhia mkataba huo sasa.

“Tanzania kuingia kwenye mkataba huu manufaa ni makubwa sana, tukiingia tuna uhakika wa soko kubwa la zaidi ya watu bilioni moja. Mchakato mzima wa kuridhia mkataba umefikia mwisho inayosubiriwa ni hatua ya mwisho ili turidhie na kusaini, hatutachukua muda mrefu,” alisema.

Chanzo: ippmedia.com