Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkandarasi skimu ya umwagiliaji apewa siku saba

Kilimo Kilimanjaro Mkandarasi skimu ya umwagiliaji apewa siku saba

Fri, 15 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kufuatia kusuasua kwa mradi wa ujenzi wa skimu ya umwagiliaji katika Kata ya Kwa Mndolwa wilayani Korogwe mkoani Tanga, Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amempa siku saba mkandarasi anayesimamia mradi huo kupeleka vifaa husika kwa ajili ya kuukamilisha kwa wakati ambao umepangwa.

Waziri Bashe amesema mkandarasi huyo amepewa mkataba wa mwaka mmoja, lakini hadi sasa ametumia miezi sita huku mradi huo ukiwa asilimia 20, jambo ambalo haliridhishi.

Katika hatua nyingine, amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, William Mwakilema kumsimamia mkandarasi huyo kwa kufika eneo la mradi kila wakati na kuongeza kuwa endapo kasi itaendelea kuwa chini, hatua za kisheria zichukuliwe.

Skimu hiyo inatarajiwa kunufaisha vijiji vya Kwa Mndolwa, Mahenge, Kerenge na Kibaoni ambapo Serikali imetenga shilingi bilioni 1.85 kukamilisha mradi huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live