Kamishna Idara ya PPP Wizara ya Fedha na Mipango, David Kafulila ametanabaisha juu ya hali ya Ongezeko la Deni katika nchi na Dunia, lakini pia Kwa jinsi Serikali inavyoingia Ubia na makampuni Binafsi.
"Ili Serikali iweze kutumiza matarajio ya wananchi katika nchi au Duniani, na ndio maan Dunia inakuja na msukumo mkubwa sana, kwamba Sekta Binafsi ifanye mambo ambayo Serikali ingeweza kuyafanya"
"Hapa Juzi Serikali imefungua utaratibu wa Kujenga Barabara ya Kibaha, Chalinze mpaka Morogoro kujengwa Kwa utaratibu wa Ubia, Kwa maana ya kwamba tunaalika kampuni Binafsi kujenga hiyo Barabara (Express Four Way) yaani babarara nne, kutoka Kibaha Hadi Chalinze na baadae Hadi Morogoro.
"Hii itapunguza msongamano au muda ambapo mtu angesafiri hicho kipande, Uamuzi huu utapunguza msongamano, na ni dhahiri kuwa Barabara ya Kawaida itakuwepo kama kawaida."