Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkaguzi alalamika risiti za EFD kufutika haraka

88792 Efd+pic Mkaguzi alalamika risiti za EFD kufutika haraka

Tue, 17 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Ofisa kutoka ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) amekiri changamoto wanazopata kutokana na risiti za EFD ikiwamo maandishi yake kufutika haraka.

Ofisa huyo wa ofisi ya CAG, Renatus Leonard ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Desemba 16, 2019 wakati akiwa kwenye warsha ya siku mbili kwa asasi zisizo za kiserikali na waandishi wa habari kuhusu kuzijua taarifa za ukaguzi na tafsiri zake.

Akijibu swali kuhusu ubora wa risiti, amesema mara kadhaa wametoa mapendekezo kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) lakini mapendekezo yao hayajafanyiwa kazi.

"Ni muhimu sana kuniridhisha lakini tusaidieni hata ninyi wananchi, risiti zile zinachangamoto kubwa, zinafutika baada ya muda na kupoteza uhalisia," amesema Leonard.

Katika hatua nyingine ofisa huyo amesema ofisi ya CAG ingetamani kuwakagua, kuwakamata, kuwapeleka mahakani na kuwafunga kwa haraka watu ambao wametumia vibaya mali ya umma lakini utawala bora unawabana.

Amesema Tanzania inafuata misingi ya utawala bora hivyo wanachokifanya wao ni kukagua na kutoa taarifa yao lakini lingine zaidi ya hapo hawana.

Awali Naibu CAG, Benjamini Mashauri amesema mwamko wa Watanzania katika kutuatilia ripoti za ukaguzi umekuwa mkubwa jambo linaloonyesha wengi wanataka kujua fedha zao zinatumikaje.

Chanzo: mwananchi.co.tz