Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mizigo ya Zambia kukaa nchini siku 45 bure

Samia Hichilema Mizigo ya Zambia kukaa nchini siku 45 bure

Thu, 26 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

li kuvutia wafanyabiashara zaidi kutoka Zambia kutumia Bandari ya Dar es Salaam pamoja na kuwapunguzia gharama za kupitisha mizigo yao Tanzania, Serikali ya Tanzania imeongeza muda ambao wafanyabiashara wa Zambia wataweka mizigo yao nchini bila kulipia kwa siku 30.

Ongezeko hilo linafanya idadi ya siku ambazo mizigo itakaa bure kutoka 15 katika Bandari ya Dar es Salaam hadi siku 45 katika Bandari Kavu ya Kwala mkoani Pwani ambapo Zambia imetengenewa eneo la hekta 20 kwa ajili ya kuhifadhi mizigo.

Akizungumza mapema leo, Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema amemshukuru Rais Samia Suluhu kwa zawadi hiyo na kuahidi kuwa ni watalitumia eneo hilo walilotengewa kama zawadi ya maadhimisho ya miaka 59 ya uhuru wao.

Rais Samia alikuwa nchini Zambia kwa ziara ya kitaifa ya siku tatu kuanzia Oktoba 23 hadi Oktoba 25 kwa mwaliko wa mwenyeji wake, Rais Hichilema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live