Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Miwa yageuka dili soko la Tandale

Miwa Sugar Cane Miwa yageuka dili soko la Tandale

Thu, 24 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KWA kipindi cha miaka mitatu maeneo yanayoingiza miwa katika Soko la Tandale yameongezeka kutoka manne hadi kufikia sita. - Mjumbe wa Kitengo cha Miwa katika Soko la Tandale, Hamis Kinugwa alisema jana kuwa ongezeko hilo linatokana na kuwa mwanzoni miwa ilitoka katika maeneo ya Korogwe, Muheza mkoani Tanga, Morogoro na Kigoma lakini hivi sasa inatoka Wilaya ya Gairo, Morogoro na Kilindi mkoani Tanga. - Alisema mahitaji ya bidhaa hiyo ni makubwa kwa kuwa wajasiriamali wadogo wa kuuza miwa kwa kusukuma mikokoteni pamoja na wakamuaji wa juisi ya miwa mkoani Dar es Salaam ndio wateja wao wakubwa. - Alisema Oktoba mpaka Machi ndio kipindi bidhaa hiyo inauzika zaidi kwa kuwa ni msimu wa joto, lakini matunda mengine yanakuwa yamepungua. - Alisema kwa sasa fungu moja la miwa lenye miwa 20 huuzwa kati ya Sh 8,000 hadi 10,000 kutegemeana na upatikanaji wake kwa kipindi hicho. - Alisema katika soko hilo magari huingia kutegemeana na mahitaji yalivyo kwani kuna siku magari hayaingii kabisa endapo bado kuna miwa mingi, ama yanaingia kati ya mawili hadi 10.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live