Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Miundombinu wezeshi muhimu uchumi wa kidijitali

83cef24590b69c16485a174b196ed35c Miundombinu wezeshi muhimu uchumi wa kidijitali

Tue, 8 Feb 2022 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Uchumi wa kidijitali utafikiwa endapo tutajenga miundombinu wezeshi. Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano na Mfumo wa Anwani za Makazi ni moja ya miundombinu wezeshi inayotekelezwa na Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,Nape Nnauye leo mjini Dodoma, katika kikao kazi cha Wakuu wa Mikoa kuhusu kufanikisha utekelezaji wa mfumo wa anwani za makazi nchini ifikapo mwezi Mei mwaka huu.

Amesema kwa upande wa Mkongo serikali imefikia asilimia 55 ya lengo la 2025 ambapo zimejengwa kilomita 8,300 kati ya kilomita 15,000 zitakazotimiza lengo la kila mwananchi kupata intaneti ya kasi.

“Mheshimiwa Rais, kwa upande wa Anwani za Makazi ilipangwa kufikia 2025 jumla ya kata 4067 ziwe zimewekewa miundombinu ya anwani za makazi.” amesema

Amesema hadi sasa utekelezaji umefanyika katika kata 135 ambayo ni sawa na asilimia tatu tu na kukiri kuwa kasi ni ndogo ndio uliopelekea uamuzi wa kubadili mkakati wa utekelezaji.

Amesema manufaa makubwa yatakayopatikana katika kufanikisha anuani ya makazi mwezi Mei mwaka huu, utakuwa na tija katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi inayotarajiwa kufanyika Mwezi Agosti, 2022.

Aidha Nape, amesema tayari Wizara imejenga uwezo kwa watendaji na wataalamu wa Mikoa na Halmashauri zote nchini (196 za Tanzania Bara na Zanzibar) kuhusu utekelezaji na Matumizi ya Programu Tumizi ya Mfumo.

Nape amesema “Nikushukuru tena Mhe Rais kupata nafasi ya kuungana nasi katika jitihada hizi. Mheshimiwa Rais, Dhamira ya Wizara ninayoiongoza kwa kushirikiana na wadau wengine ni kuhakikisha kuwa kila mwananchi anakuwa na Anwani ya Makazi ifikapo Mwezi Mei, 2022.

Ukamilishaji huu pamoja na manufaa makubwa yatakayopatikana, utakuwa na tija katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi inayotarajiwa kufanyika Mwezi Agosti, 2022.

Wizara tayari imejenga uwezo kwa watendaji na wataalamu wa Mikoa na Halmashauri zote nchini (196 za Tanzania Bara na Zanzibar) kuhusu utekelezaji na Matumizi ya Programu Tumizi ya Mfumo.

Wataalam hawa watawajengea uwezo watendaji wa Vijiji/Mitaa ambao watatumika katika kukusanya taarifa za Anwani za Makazi na kutoa Anwani husika kwa Wananchi.

Amesema Wizara imeandaa mratibu na mtaalam wa Mfumo huu, tunaahidi kutoa ushirikiano kwa viongozi katika ngazi zote na wadau wote kuhakikisha kila mwananchi anakuwa na Anwani ya Makazi katika muda uliopangwa ili manufaa ya Mfumo huu yaonekane na kuleta tija kwa wananchi.

“Ili kutekeleza hili, tumeandaa Mwongozo ili kurahisisha utekelezaji katika Halmashauri. Aidha, kupitia bajeti ya Wizara yangu ya mwaka 2021/22 tulitengewa kiasi cha shilingi Bilioni 45 hata hivyo hadi kufikia mwezi Februari Wizara imepokea kiasi cha shilingi Bilioni 13,274,770,613.00 kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa mradi.” Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,Nape Nnauye leo mjini Dodoma, katika kikao kazi cha Wakuu wa Mikoa kuhusu kufanikisha utekelezaji wa mfumo wa anwani za makazi nchini ifikapo mwezi Mei mwaka huu.

Amesema kiasi cha shilingi bilioni 28 zitagawanywa katika mikoa yote Bara na Zanzibar kwa ajili ya kuwezesha utekelezaji kwa haraka na tija.

Chanzo: www.habarileo.co.tz