Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mitungi ya gesi kutolewa bure

GESII WEBB Mitungi ya gesi kutolewa bure

Wed, 3 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

JUMLA ya mitungi 100,000 inatarajiwa kutolewa bure ifikapo mwezi Julai,2023 katika maeneo ya vijijini nchi nzima, ikiwa ni hatua ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi. - Mpango huo umekuja mara baada ya serikali kutenga kiasi cha Sh Bilioni 3.2 kwa mwaka wa fedha 2022/2023 kwa ajili ya usambazaji wa gesi safi ya kupikia. - Mkurugenzi wa Uenezaji Masoko na Teknolojia Kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Advera Mwijage amesema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokutana na wadau wa gesi nchini na kueleza kuwa wameshaanza kuweka fomu ya maoni tangu Aprili 19 na kukamilishwa Mei,10,2023, ili kupata watu watakaonufaika na gesi hizo. - “Tumefanya kikao na wasambazaji wa mitungi ya gesi na kwa hapa Tanzania sasa tuna kampuni 11 na bahati nzuri wote wamefika na ujumbe wetu kwao ni wao kuwa tayari kushirikiana na serikali kuhakikisha kwamba tunasaidiana kwenye usambazaji wa nishati safi na salama maeneo ya vijijin,”ameeleza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live