MKUU wa Mkoa wa Shinyanga, Christina Mndeme amezindua na kuwasha mitambo iliyozimwa baada ya kusitisha uzalishaji kwa kipindi cha miezi minane kwenye kampuni ya Williamson Diamond inayochimba madini ya almas iliyopo Mwadui wilayani Kishapu mkoani hapa.
Hatua hiyo ni utekelezaji wa agizo la kuanza uzalishaji lilitolewa na Waziri wa Madini, Dotto Biteko baada ya kutembelea ujenzi wa bwawa tope jipya takribani wiki mbili zilizopita.
Mndeme alisema hayo jana wakati akiongoza zoezi la kuwashwa mitambo huku alitoa maelekezo kwa uongozi wa mgodi kuanzisha bwawa lingine la dharura pindi inapotokea majanga mgodi usisimame kama ilivyokuwa na kuleta hasara.
“Kweli kampuni na serikali zimepata hasara kwa kipindi cha miezi nane siku nilipofika hapa kuona ujenzi wa bwawa unavyoendelea nikatoa maagizo mfanye kazi usiku na mchana haina tarehe moja mwezi Agost uzalishaji uanze lakini mmefanya kazi nzuri kabla ya tarehe hiyo uzalishaji umeanza hongereni sana”alisema Mndeme.a