Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Misri yawekeza Shilingi trilioni tatu yazalisha ajira 2,206

788d579a7af3b7885931dd62c65b9096 Misri yawekeza Shilingi trilioni tatu yazalisha ajira 2,206

Wed, 2 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Misri imesema nchi hiyo imewekeza nchini Tanzania kwenye miradi 26 yenye thamani ya shilingi trilioni 3.1 na kutengeneza ajira 2,206 kwa Watanzania.

Balozi wa Misri nchini Tanzania, Mohamed Gaber Abulwafa alisema hayo Dar es Salaam alipokutana na kuzungumza na Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dk Ashatu Kijaji.

Abulwafa alisema wawekezaji kutoka Misri walifika nchini Tanzania katika Kongamano la Biashara lililofanyika nchini Tanzania wakapata fursa za kuwekeza.

Alisema kwa sasa wanaendelea na taratibu kuja kuwekeza Tanzania katika sekta ya kilimo na mifugo hasa biashara ya korosho, parachichi na Mahindi.

Aidha alisema Misri ipo katika hatua za ukamilishwaji wa kuanza kwa usafiri wa abiria kwa njia maji kutoka Misri hadi Tanzania ili kukuza uwekezaji na biashara na kurahisha usafirisjhaji wa bidhaa katika nchi hizo mbili.

Alisema Misri imekuwa ikitekeleza miradi ya kimkakati katika nchi ya Tanzania ukiwemo ujenzi wa mradi wa Bwawa la Kufua Umeme wa Maji la Julius Nyerere (JNHPP) unaotarajiwa kukamilika Juni mwaka huu na kuzalisha megawati 2115.

Dk Kijaji alisema uhusiano na ushirikiano wa uwekezaji baina ya Misri na Tanzania umekuwa ukiimarika zaidi baada ya ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan aliyoifanya Misri Novemba 10 mwaka jana ambako alikutana na Rais wa nchi hiyo, Abdel Fattah Al Sisi. Alisema hivi sasa biashara baina ya nchi hizo mbili imeongezeka kutoka shilingi bilioni 84.3 mwaka 2018 hadi kufikia shilingi bilioni 87.3 mwaka 2020.

Dk Kijaji alisema kwa kuzingatia hilo kuna umuhimu wa kuendeleza majadiliano na makongamano ya biashara baina ya nchi hizo ili kutoa fursa kwa wafanyabiashara kutumia fursa za uwekezaji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live