Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Misitu 20 Kilosa kutambuliwa kimataifa, kuingizwa kwenye kanzidata ya dunia

MSITU Kilosa Misitu 20 Kilosa kutambuliwa kimataifa, kuingizwa kwenye kanzidata ya dunia

Tue, 8 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja Mradi wa Mkaa Endelevu wa Shirika la Kuhifadhi Misitu Asilia Tanzania (CoForEST-TFCG), Charles Leonard amesema kwa sasa shirika lipo kwenye mchakato wa misitu 20 ilivyohifadhiwa kwenye vijiji wilaya ya Kilosa mkoani kutambulika kimataifa na kusajiliwa kwenye ngazi ya Umoja wa Mataifa ya kanzidata ya maeneo yaliytohifadhiwa kidunia.

Amesema mchakato huo upo katika hatua za mwisho na Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imesharidhia na kwamba mwezi Februari mwaka huu 2022 misitu hiyo itafahamika rasmi kidunia kama misitu iliyohifadhi ya vijiji.

Amesema hayo mbele ya kamati ya Siasa ya Chama Cha Mpinduzi (CCM) wilayani Kilosa ilipotembelea msitu wa Kijijiji cha Chabima ambapo kamati hiyo ilikuwa ikikagua miradi ya maendeleo kijiji hapo ukiwemo mradi wa mkaa endelevu unaosimamiwa na Shirika la Kuhifadhi Misitu asilia Tanzania(TFCG) pamoja na Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania(MJUMITA).

Leonard amesema faida za misitu hiyo kuwa kwenye kanzidata hiyo kutambulika kimataifa kwani kuwepo kwa misitu kutawezesha vijiji kujitegemea kiuchumi vyenyewe badala ya kutegemea Serikali katika kila miradi mbalimbali ya maendeleo.

“Wafadhili wanaelekeza fedha zao kuja kwenye misitu hii ili kuendelea kuhifadhiwa kwani maeneo mengi duniani misitu imetoweka na hivyo kusababisha mabadiliko ya tabia nchi kama ukame ndo maada wanataka misitu iliyopo ilindwe na kutunzwa,”amesema Leonard.

Amesema Banki ya Dunia ilifanya utafiti mwaka 2007 mpaka 2009 ikaonekana upotevu wa zaidi ya Sh 100 bilioni kila mwaka kutokana na rasilimali za sekta ya mkaa, na mchango wa sekta ya mkaa kwenye pato la taifa ni dola 1 bilioni sawa na zaidi ya Sh2.2 tirioni kwa mwaka na kwamba hiyo ni zaidi ya mazao makubwa yakiunganishwa ikiwamo korosho, mkonge na mengineyo.

Advertisement Mradi wa mkaa endelevu umejikita katika misitu ya hifadhi ya vijiji sio ile misitu ya Serikali Kuu na iliyokuwa haijaifadhiwa imekuwa ikiwezeshwa kuhifadhiwa na kwamba kumekuwa na mpango wa kusimamia msitu kwa sheria ndogo zinazopitishwa na baraza la madiwani.

Katibu wa kamati ya Maliasili katika kijiji cha Chabima, Iddi Tangula amesema kuwa pamoja na msitu huo wa kijiji kuwa na faida ikiwemo kuwawezesha kujenga Zahanati, vyumba vya madarasa shule ya msingi, ujenzi wa madarasa ya Sekondari bado kumekuwepo na chanagamto  mbalimbali ikiwemo ya uvamizi wa msitu kwa watu kufanya shughuli za kibinadamu kama Kilimo na Ufugaji.

Katibu wa CCM wilaya ya Kilosa akizungumza kwa niaba ya wajumbe wa kamati ya siasa, amewataka kamati za maliasili za vijiji vilivyohifadhiwa kufanya doria za mara kwa mara ndani ya misitu na kuwafichua wale wote wanaoendelea kufanya uhalibifu wa msitu kwa kuchoma moto ovyo, kuchoma mkaa kiholela na kukata miti kinyemela.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live