Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Misamaha ya kodi yatolewa kuvutia uwekezaji nchini

Uchumi Kupanda Misamaha ya kodi yatolewa kuvutia uwekezaji nchini

Tue, 30 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Gilead Terry amesema serikali ya awamu ya sita (6) imetoa misamaha mingi ya kodi na kuweka vivutio vingi vya uwekezaji ili kuvutia zaidi Watanzania na wageni wengi zaidi kuwekeza kwenye sekta ya utalii nchini

Terry amesema hayo wakati akizungumza na wanahabari nje ya ukumbi wa mikutano Grand Melia kabla ya kuanza kwa kongamano la uwekezaji kwenye sekta ya utalii, mkoani Arusha

Terry amewaambia wanahabari kuwa lengo la kongamano hilo ni kuwajulisha wadau wa sekta ya utalii kuhusu fursa hizo za utalii na nafuu mbalimbali zilizowekwa na serikali kupitia sheria ya uwekezaji ya mwaka 2022

Kongamano hilo pia kulingana na TIC, litakuwa na majadiliano na wadau waliopo kwenye sekta ya utalii mkoani Arusha ili kujua fursa na changamoto zilizopo ili kuongeza kiwango cha uwekezaji kwenye sekta hiyo

Kongamano hili linalofanyika leo, Aprili 29, 2024 linaongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo kwa kushirikiana na Waziri wa Maliasili na Utalii Angela Kairuki

Kongamano hilo linafuatia maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyotoa wakati akiwaapisha viongozi mbalimbali akimtaka Mkuu wa mkoa wa Arusha Paul Makonda kushughulikia changamoto ya upatikanaji wa vyumba vya kulala wageni wanaotembelea mkoa wa Arusha

Chanzo: www.tanzaniaweb.live