Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Miradi yazalisha ajira 160,107, mauzo ya bidhaa yapaa

Ajira Mpyaaaaa Miradi yazalisha ajira 160,107, mauzo ya bidhaa yapaa

Mon, 6 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imesema jumla ya ajira 160,107 zimezalishwa kutokana na miradi 883 iliyowekezwa nchini katika kipindi cha kati ya Juni 2021 na Septemba 2023.

Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo ameyasema hayo leo Jumatatu Novemba 6, 2023 wakati akiwasilisha Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2024/25.

Amesema katika kukuza biashara na uwekezaji pamoja na hatua zingine, Serikali iliendelea kuweka mazingira mazuri ya biashara na uwekezaji ambapo miradi hiyo ilikuwa na thamani ya Dola za Marekani yenye milioni 12,154 ilisajiliwa katika Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).

Aidha, katika kuimarisha uwezo wa uzalishaji viwandani, kiwango cha mauzo ya bidhaa za viwandani kiliongezeka kwa asilimia 20.8, kutoka Dola za Marekani milioni 1,109.3 mwaka 2021 na kufikia Dola za Marekani milioni 1,340.5 mwaka 2022.

Amesema baadaye kiwango hicho kiliongezeka na kufikia Dola za Marekani milioni 1,401.2 mwaka 2023.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live