Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mipango yasukwa uwekezaji nsekta ya madini nchini

Madini Pic Data Mipango yasukwa uwekezaji nsekta ya madini nchini

Thu, 5 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wizara ya Madini imeweka Mipango ya kuhakikisha Sekta Madini inafungamanishwa na mipango ya taifa ili kuwa na Matumizi yenye tija katika rasilimali za nchi hususani katika Sekta ya Madini.

Hayo yameelezwa Oktoba 4, 2023 na Waziri wa Madini, Anthony Mavunde alipokutana na Waziri Ofisi ya Rais Uwekezaji na Mipango, Prof. Kitila Mkumbo wakati wa kikao kifupi kilicholenga kujenga mahusiano mazuri ya uwekezaji nchini Ofisi za Wizara ya Madini Jijini Dodoma.

Amesema ushirikiano wa Wizara hizo mbili utaimarishwa ili Sekta ya Madini iweze kuingizwa katika mipango yenye tija kwa taifa na hatimaye kukuza uchumi wa madini.

Waziri Mavunde amesisitiza kuwa madini ni sayansi hivyo Sekta ya Madini itahakikisha inafanya utafiti wa madini nchini kupitia Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) ili kuvutia wawekezaji nchini.

Kwa upande wake Prof. Kitila Mkumbo ,amesema Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji inaratibu na kuweka mazingira mazuri yanayoratibika kwa uwekezaji katika Taasisi za Umma

Ameongeza kuwa, kuhusu Madini Muhimu na Madini Mkakati Prof. Kitila amesisitiza mahitaji ya madini hayo duniani iwe chachu kwa Tanzania kutumia fursa hiyo katika kujenga mazingira bora ya kiuchumi ikiwa pamoja na kuibua maeneo mapya ya uwekezaji.

Pia, Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango Wizara ya Madini Angelo Haule amesema mapendekezo ya Vipaumbele kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 ni kuendelea kufanya utafiti wa jiofizikia kwa kutumia ndege (High Resolution Airborne Geophysical Survey) na kuimarisha mifumo ya ukusanyaji maduhuli na utoaji wa leseni.

Vile vile, Mtendaji Mkuu wa GST, Dkt. Mussa Budeba amesisitiza kuwa, kama Dira 2030 ya wizara Madini ni Maisha na Utajiri Sekta ya Madini itafanya utafiti ili kufikia maeneo mengi nchini na kuwawezesha wachimbaji wadogo kuchimba kwa tija badala ya kubahatisha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live