Zaidi ya Milioni 800 zimetolewa kwa vikundi vya wajasiriamali kwa Mkoa wa Arusha kwa lengo la kuwaongezea mitaji pamoja na kuwawezesha kufungua viwanda vidogo vidogo kupitia shirika la viwanda vidogo SIDO.
Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Arusha meneja wa Mfuko wa hifadhi ya jamii Josephat Komba wakati wa maonyesho ya wajasiriamali kanda ya kaskazini yaliyoandaliwa na SIDO.
Komba anasema wameshiriki maonesho hayo kwa lengo la kutoa elimu kwa wajasiriamali juu ya suala la kukuza mitaji yao ili kuweza kuondokana na changamoto ya ukosefu wa mitaji kwa wajasiriamali hao.
"Kuna mikopo kwa wajasiriamali ambao wanajiunga na Nssf kwa hiari ambapo mikopo hii inaratibiwa na baraza la uwezeshaji wananchi kiuchumi pamoja na Sido wenyewe "Alisema Komba
Ameongeza kuwa ili mjasiriamali apate nafasi ya kunufaika na mikopo hiyo anapaswa kujiunga kuwa mwanachama wa NSSF ambapo atapata nafasi ya kuomba kupewa mkopo wenye masharti nafuu ambao utamuwezesha kufungua viwanda vidogo na vya kati.