Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema kwa mwaka huu Serikali imekumbana na changamito ya baadhi ya Wafanyabiashara kutafuta njia ya kutorosha mbolea kwa kuwa walishindwa kuiba ndani ya mfumo na hivyo wakatafuta namna ya kuitorosha.
Ameitaja mikoa ya Songwe na Kigoma kuwa ndio iliyoisumbua zaidi Serikali katika changamoto hiyo, na kuongeza kuwa Serikali imewakamata baadhi ya Wafanyabiashara waliokuwa wakitorosha mbolea hiyo na tayari wamefikishwa mahakamani.
Waziri Bashe ameyasema hayo Bungeni, Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina aliyedai kuwa kwa msimu uliopita mfumo wa usambazaji wa mbolea uligubikwa na changamoto nyingi na kutaka kufahamu Serikali imejipanga vipi kutatua changamoto hizo kwa msimu huu.