Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mikataba bandari ya Bagamoyo na 'eti eti ' zake

Bandari Bagamoyo (600 X 353) Mikataba bandari ya Bagamoyo na 'eti eti ' zake

Tue, 31 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Serikali ikieleza nia ya kuendeleza mradi wa Bandari na Kanda Maalumu ya Kiuchumi Bagamoyo (BSEZ), baadhi ya wadau wametahadharisha mikataba na wabia wa mradi huo.

Akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kwa mwaka 2022/23 Mei 6, Waziri Dk Ashatu Kijaji alisema wizara imefufua majadiliano na kampuni za China Merchants Holdings International Co. Ltd (CMHI) na Oman Investment Authority (OIA) ambayo awali ilikuwa inaitwa Mfuko wa Uwekezaji wa Serikali ya Oman (SGRF).

Awali, mradi huo ulioanzishwa mwaka 2015, ulishindwa kuendelea baada ya hayati Rais John Magufuli kutilia shaka mkataba wa ujenzi wa bandari hiyo.

Hata hivyo, Juni 26, 2021 Rais Samia aliweka wazi dhamira ya kuendeleza mradi huo sambamba na ule wa chuma na makaa ya mawe wa Mchuchuma na Liganga, wakati akizungumza na wajumbe wa Baraza la Taifa la Biashara (TBNC) Dar es Salaam.

Akizungumza na Mwananchi kwa simu hivi karibuni, mhadhiri wa uchumi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Abel Kinyondo alisema licha ya manufaa ya bandari hiyo, Serikali inapaswa kuwa makini na mikataba ya wabia watakaoiendeleza bandari hiyo, zikiwamo kampuni za China.

“Sisi hatutakuwa nchi ya kwanza kujengewa bandari na China au miundombinu ya usafiri. China imejenga bandari nyingi, viwanja vya ndege vingi na reli nyingi duniani,” alisema Dk Kinyondo.

Advertisement “Kama watu wanapiga kelele, kuwanyamazisha wangekuwa wazi, kwamba bwana kama unavyosema hayo sio ukweli, mkataba ni huu hapa.

“Unapoonyesha mkataba sio lazima kuonyesha kila kitu kwa undani, mkataba una mambo mengi, kuna vifungu vya ujumla na mambo mahsusi kama vile mnalipanaje,” alisema.

Hivi karibuni wakati akitambulisha ujumbe wa kampuni 40 kutoka nchi hiyo zinazosaka fursa za uwekezaji nchini, Balozi Nabil Hajloui alisema bandari ya Bagamoyo ni miongoni mwa fursa hizo.

Makamu mwenyekiti wa kamati ya Afrika ya shirikisho la waajiri wakubwa nchini Ufaransa, Gerard Wolf alizungumzia uwekezaji wa bandari akisema changamoto iliyopo ni pamoja na kudhibiti uchafuzi wa mazingira, ikiwemo hewa ukaa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live