Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mikakati yaanza Kigoma kuwa kitovu cha biashara Maziwa Makuu

56733 Pic+biashara

Mon, 13 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kigoma. Mkoa wa Kigoma unaweza kutumika kama kituo kikuu cha biashara katika ukanda wa nchi zinazozunguka Ziwa Tanganyika na kuwafanya raia wa nchi jirani kununua bidhaa mkoani hapa.

Kauli hii ilitolewa jana na mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji tanzania (TIC), Geofrey Mwambe, kwenye kongamano la biashara linalofanyika mjini Kigoma.

Kongamano hilo linahusisha wafanyabiashara na wawekezaji kutoka nchi za Tanzania, Zambia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Burundi na Rwanda wanajadili njia bora ya kuboresha biashara na kukuza uchumi.

Hata hivyo, Mwambe aliwataka wafanyabiashara wa Kigoma kuwa mstari wa mbele kutumia fursa ya uwekezaji badala ya kusubiri wageni.

Naye mkuu wa mkoa huo, Emmanuel Maganga alisema wamejipanga kuhakikisha fursa za uwekezaji na biashara zinatumika ipasavyo na uchumi unakuwa kwa kasi.

“Wawekezaji njooni Kigoma kuna fursa nyingi na nzuri kwani ardhi ipo ya kutosha na yenye rutuba, miundombinu ya usafiri na usafirishaji ipo vizuri,” alisema Maganga.

Pia Soma

Naibu waziri wa Tamisemi, Josephart Kandege alisema kauli mbiu ya ‘mipaka yetu na maendeleo’ ikitumika vizuri itasaidia kuinua uchumi katika nchi za maziwa makuu.

Chanzo: mwananchi.co.tz