Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mifumo ya malipo kuboreshwa zaidi

Fedhapic Mifumo ya malipo kuboreshwa zaidi

Fri, 22 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Changamoto ya mifumo kutokusomana kwa haraka hasa katika maeneo ya bandari na mipakani kwenye mamlaka ya forodha kulionekana kukwamisha baadhi ya shughuli za malipo na kuchelewesha shughuli za kibiashara.

Hayo yamebainishwa na baadhi ya wafanyabiashara jijini Dodoma ambapo wameishauri serikali kuboresha mifumo iliyounganishwa katika utoaji huduma ili kuwarahisishia kufanya malipo kwa haraka.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu Serikali Mtandao ameiambia #EastAfricaRadio kuwa wameendelea kushughulikia changamoto mbalimbali zilizokua zikijitokeza katika mifumo inayotumika katika forodha mbalimbali hasa kwenye njia kuu za mifumo ya biashara ikiwemo bandarini na mamlaka za forodha za mipakani.

Katika hatua nyingone Eng.Ndomba amewatoa wasiwasi watumiaji wa mifumo hiyo kuwa ni salama na haiwezi kuingiliwa au kupoteza kumbukumbu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live