Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mifuko ya hifadhi ya jamii yaaswa kuwekeza TDB

E0EFD0FB E2CA 47A8 AB7B 6353AB3DD49C.jpeg Mifuko ya hifadhi ya jamii yaaswa kuwekeza TDB

Sat, 15 Oct 2022 Chanzo: eatv.tv

Mifuko ya hifadhi ya jamii imetakiwa kuona fursa zinazopatikana katika nchi wanachama ambao Tanzania ni mwanachama wake ili kuiletea nchi maendekeo kutokana na magawio yanayotolewa.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa hifadhi ya Jamii kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, vijana, ajira na wenye ulemavu Bw. Festo Fute alipokuwa akizungumza wadau wa uhifadhi wa jamii katika mkutano uliowakutanisha na Wawakilishi wa benki iliyopo chini ya Somo kuu la kusini na mashariki mwa Afrika ili kuona namna ya kuweza kuwekeza katika benki hiyo.

"Hifadhi za jamii zikitumika vizuri na zikawekeza na kupata ubia katika taasisi za kijumuiya na kikanda Tanzania tutapata mafanikio makubwa katika kupambana na umakini, lakini pia mfano tuna benki ya Afrika, tuna Benki ya Maendeleo ya Kusini na Mashariki mwa Afrika ambayo kama wote wakiwekeza huku na kupata hisa maana yake ni kwamba kama nchi ambayo ni mwanachama tutapata sifa ya kukopa kwenye taasisi hizi na kuwekeza katika miradi ya maendeleo. Mifuko kama NSSF kwamfano wamewekeza dola Mil. 11 na kupata share ya 8% ambapo hapa tayari tumepata sifa ya kupata mkopo kutoka TDB. Kumbe mifuko yote ikiwekeza huku tutapata maendeleo makubwa mno"- Festo Fute - Mkurugenzi wa hifadhi ya Jamii, Ofisi ya Waziri Mkuu. 

Akizungumza kwa niaba ya TDB ambayo ni benki ya mataifa ya kusini na mashariki mwa Afrika, afisa uwekezaji amesema mifuko hiyo haitajutia kuwekeza TDB kwani Taifa litanufaika katika miradi mbalimbali ya maendekeo na kwamba wamekuwa wakishirikiana na Tanzania katika miradi ya miundombinu kama SGR na kilimo.  

Chanzo: eatv.tv