Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mifuko mbadala itasambaa baada ya Juni Mosi - Wazalishaji

59157 Mifukopic

Wed, 22 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Umoja wa wazalishaji wa mifuko mbadala umesema kutoonekana mifuko hiyo katika maeneo mengi nchini kunatokana na uwapo wa nguvu kubwa ya mifuko ya plastiki.

Hata hivyo, wanasema wana matumaini kwamba ikifika Juni Mosi, mifuko hiyo itachukua nafasi sokoni.

Wameyasema hayo leo, Jumatano  Mei 22, 2019 kwenye mkutano wa habari uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake,  Allen Kimambo amesema alianza kuwatoa hofu Watanzania na kusema umoja umezalisha mifuko mbadala ambayo ni pamoja na ya  karatasi, vitenge na vitambaa vyepesi.

“Ikifika Juni Mosi ndiyo ukomo wa katazo hili, mifuko yetu itachukua nafasi yake na tayari tumeshaanza kuisambaza. Wingi wa mifuko ya plastiki inasababisha, mifuko mbadala  kutoshika kasi .

"Kuanzia Juni Mosi wasipoiona mifuko ya plastiki, watalazimika kutumia mbadala ambayo itakuwa imesambazwa maeneo mablimbali,” amesema Kimambo.

Pia Soma

Naye Sarah Pima amewahakikishia na kutoa hofu Watanzania kuhusu upatikanaji wa mifuko mbadala aliyosema tayari imezalishwa kwa wingi.

Pia, amesema umoja huo umeanza kutoa mafunzo kwenye maeneo mbalimbali yanayolenga kuwajengea uwezo vikundi vya ujasiriamali ili vizalishe mifuko hiyo mbadala.

Chanzo: mwananchi.co.tz