Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Michezo ya kubahatisha yakuza uchumi nchini

Michezo Ya Kubahatisha Yakuza Uchumi Nchini Michezo ya kubahatisha yakuza uchumi nchini

Wed, 25 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Michezo ya kubahatisha imeendelea kuwa burudani kubwa kwa vijana wengi na sehemu ya kipato pale inapotokea mtu ameshinda ubashiri wake.

Mbali na vipato wanavyopata wachezaji wa michezo hiyo, lakini pia Serikali imekuwa ikipata mapato kutokana na kodi na tozo mbalimbali zinazolipwa na kampuni hiyo.

Kwa miongo mingi uchumi wa Tanzania umekuwa ukibebwa na sekta za kilimo, viwanda, utalii, madini, mawasiliano, biashara lakini sekta ya michezo ya kubashiri kwa miaka ya hivi karibuni imechangia pakubwa katika uchumi na pato la Taifa.

Kwa mujibu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, michezo ya kubahatisha imechangia kiasi cha Sh 170 bilioni kwenye Pato la Taifa na kuzalisha ajira 25,000 katika kipindi cha miaka 20 iliyopita.

SportPesa ni kampuni namba moja ya michezo ya kubashiri nchini, imekuwa chaguo la kwanza kwa wapenzi wa michezo ya kubahatisha nchini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live