Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgogoro wafugaji, wawekezaji Kitengule kumalizwa

Ulega Wafugaji.jpeg Mgogoro wafugaji, wawekezaji Kitengule kumalizwa

Sun, 23 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Abdalla Ulega amewahakikishia wananchi na wawekezaji wa Wilaya ya Karagwe kushughulikia haraka mgogoro wa kitalu namba moja unaopakana na kijijini cha Mushabaiguru kata ya Kihanga ili kuondoa migogoro ya mifugo kati ya wananchi na wawekezaji walioko maeneo ya Ranchi ya Kitengule

Waziri Ulega alitoa kauli hiyo katika mkutano wa hadhara na wananchi wa kata ya Kihanga wilayani humo alipotembelea miradi mbalimbali na kusikiliza kero za wananchi katika maeneo hayo kubwa ikiwa ni mgogoro huo.

Diwani wa kata ya Kihanga, Rwamuhangi Rwamugata alimuomba Ulega kuwepo namna ya kuwabadilishia mpaka walau kuondoa adha ya mifugo inayovuka mipaka hadi kuingia kwa mwekezaji na kusababisha migogoro inayokwamisha shughuli za maendeleo katika kata hiyo.

Ulega alikiri uwepo wa mgogoro na kuahidi kuwa sula hilo amelichukua kwa uzito na hatua zitachukuliwa kwa haraka ili usalama uendelee kuwepo wilayani humo.

Aidha, Ulega aliwasisitiza wananchi kufanya ufugaji wenye tija ili kupata maziwa ya kutosha kutokana na uwepo wa kiwanda cha kusindika maziwa.

Alisema kuwa serikali itajenga vitalu vitakavyotumika Kama sehemu kufanya ( BBT) Jenga kesho iliyo njema ili kuongeza kasi ya uzalishaji wa maziwa mengi kwani tayari kiwanda cha kusindika maziwa kipo na hakutakuwa na changamoto ya maziwa kutonunuliwa .

Aidha amewashauri wananchi wilayani Karagwe kuchangamkia fursa ya mradi wa kopa Ng’ombe lipa maziwa ili kumwezesha kila mwananchi kuwa na mfugo na kujiongezea kipato katika familia zao ambapo amewahakishia wananchi kuwa watakaokuwa tayari kujiunga na fursa hiyo watatambuliwa na kuundiwa ushirika wao.

Katibu Tawala Mkoa wa Kagera, Toba Nguvila kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa alisema serikali inaendelea kushirikiana na wafugaji na kuendelea kuwajengea uwezo ikiwemo kuwapa elimu ya ufugaji wenye tija .

Chanzo: www.tanzaniaweb.live