Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgogoro wa wachimbaji watua kwa naibu waziri

95b44e176be6e37477a356ea494586d5 Mgogoro wa wachimbaji watua kwa naibu waziri

Wed, 19 Jan 2022 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Naibu Waziri wa Madini, Dk. Lemomo Kiruswa ameingilia kati mgogoro wa eneo la uchimbaji madini ‘duara’ namba 22 kati ya wanachama na mwekezaji nakumtaka Mkuu wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida, Suleiman Mwenda kushirikiana na Afisa Madini kutatua kero hiyo.

Akizungumza, Jumanne, katika Kijiji cha Nkonkilangi wilayani Kungi, Dk Kiruswa alitaka mgogoro huo uwe umetatuliwa ndani ya siku saba.

“Nina kuagiza Mkuu wa wilaya kwa kushirikiana na Kaimu Afisa Madini mkoa wa Singida kutatua mgogoro huu na ifikapo tarehe 30 januari tupate taarifa kuwa hapa hakuna mgogoro,” alitoa maagizo hayo nakuongeza,

“Kati ya vitu ambavyo hatuhitaji kuviona katika sekta ni migogoro. Tunahitaji kuielea sekta hii kwa kuhakikisha hakuna migogoro ili wachimbaji wanufaike na ikitokea kuna mgogoro sumbufu unaosababisha wachimbaji kutopata rasilimali hii tutaifuta hiyo leseni.”

Amewahakikishia wachimbaji hao kuwa serikali inahitaji kuona kuwa kila mmoja anapata haki yake na kwamba Serikali haihitaji kuona wachimbaji wanagombana.

Akitoa ufafanuzi kuhusu maombi ya namna bora ya kusaidia upatikanaji wa maji Dk Kiruswa alisema wanahitaji kuainisha mahitaji yote ya vifaa hivyo na kuviweka katika mkakati wa Serikali.

Aidha, aliwaahidi wachimbaji hao kutuma timu ya wataalamu kutoka wizarani itakayosaidia kubaini miamba sahihi ya kuchimba ili kupata madini kwa wepesi.

Alisema wachimbaji wadogo katika mwaka wa fedha 2020/2021 wameuza gramu 319,000 katika soko la madini Shelui na kuweza kuingizia Serikali kiasi cha Sh 37 bilioni.

Aidha ametumia nafasi hiyo kumuomba naibu waziri huyo kuwasaidia wachimbaji hao kupata vifaa vitakavyowasaidia kuondoa maji ili waweze kuchimba dhahabu kwa njia nyepesi.

Akijibu hoja za wachimbaji Kaimu Afisa madini Mkoa wa Singida, Chone Malembo amewataka wachimbaji hao, kero walizonazo wakae kuzizungumzia ili wazitatue kwa sababu hakuna kinachoshindikana katika mazungumzo.

Malembo alibainisha sifa za kupata leseni kwa mujibu wa kifungu cha nane cha sheria ya madini kuwa ni mtua kuwa mtanzania mwenye umri usiokuwa chini ya miaka 18, hajawahi kushitakiwa na kutangazwa na mahakama kama aliyekosa, tini namba, picha mbili za paspoti na kitambulisho aidha cha udereva, kura au cha taifa.

Mmoja wa wachimbaji katika duara hilo namba 22, Zahara Abdilahi alisema kuwa kwa nini wao kama viongozi wa Ushirika wa Ukombozi hawachukui asilimia ya ofisi, hivyo anaomba leo hilo lipatiwe ufumbuzi.

Samora Omari anayedaiwa kuwa mwekezaji wa duara namba 22 kuhoji kuwa ninani anastahiki kuwa na leseni ya kuchimba madini kwa kuzingatia sheria za nchi ya Tanzania.

Chanzo: www.habarileo.co.tz