Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgodi wa almasi Mwadui waanza kazi

MGODI WA MWADUI Mgodi wa almasi Mwadui waanza kazi

Mon, 17 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kufuatia agizo la waziri wa madini Mheshimiwa Dotto Biteko kuwa ifikapo July 15, 2023 mgodi wa Williamson Diamond Limited kuanza rasmi kwa shughuri za uzalishaji wa madini mara baada ya kusimama kwa kipindi cha miezi 8 kufatia kubomoka kwa bwawa la kuhifadhia maji tope ndani ya mgodi na kusababisha uhalibifu wa makazi ya watu waishio pembezoni mwa mgodi huo.

Meneja Mkuu wa Mgodi wa Williamson Diamond Ltd, Mhandisi Ayubu Mwenda ameeleza namna kusitishwa kwa uzalishaji kwenye mgodi huo kulivyo athiri ukusanyaji wa mapato ya serikali ikiwemo mapato ya ndani ya halmashauri ya wilaya hiyo pamoja na kuingizia hasara kampuni.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Shinyanga aliyefika mgodini hapo kujionea namna uzalishaji unavyoendelea amewasihi uongozi wa mhgodi huo kuongeza kasu ya uzalishaji na kuzingatia utunzaji wa mazingira ikiwemo upandaji miti kwenye maeneo yanayozunguka mgodi huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live