Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgodi mdogo wafungwa baada ya kuwepo viashiria vya hatari

MGODI Mgodi mdogo wafungwa baada ya kuwepo viashiria vya hatari

Mon, 27 Apr 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ofisa Madini mkazi wa Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Joseph Kumburu, aliufunga mgodi huo jana, wakati alipotembelea migodi midogo ya Ntambalale Wisolele na Kakola namba mbili na tisa kukagua utoroshaji wa madini na uchimbaji madini salama.

Amesema kuwa, anasimamisha shughuli za uchimbaji katika mgodi huo, kwa muda wa siku saba ili viongozi wake waweze kupata muda wa kurekebisha sehemu zote hatarishi ambazo zinaweza kusababisha maafa na mpaka kufikia Aprili ,30 wawe wamekamilisha.

Kumburu amesema sababu ya kusitisha shughuli za uchimbaji wa mdogo huo,wachimbaji wamesogeleana, hakuna usalama kwa wachimbaji, hawana vifaa vya kijikinga na hatari wakati wakiendelea na shughuri za uchimbaji na wanatakiwa kuwa zaidi ya mita moja shimo moja hadi lingine.

Amesema eneo hilo lina leseni ya mwekazaji ambae muda wowote anaweza akajitokeza na kuwaondoa na kusababisha kuibuka kwa mgogoro ambao hauna tija, nakuwataka viongozi wa mgodi huo kumtafuta mwekezaji na kuzungumza nae ili awaruhusu kuendelea na uchimbaji.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wisolele Gold Mining Hamisi Mabubu, amesema kwa muda uliotolewa wa siku saba,atahakikisha anarekebisha sehemu zote zenye hatari katika mgodi huo ili kumuweka mchimbaji katika hali ya usalama wakati akiendelea na uchimbaji.

Amesema kuwa,eneo hilo walikabishiwa na serikali ya kijiji cha Wisolele kwa barua lakini kwasasa wameshafanya mazungumzo na mmiliki wa eneo hilo mwenye leseni ili waweze kuwapatia nafasi ya kuendelea kuchimba bila kuwepo kwa mgogoro baina yao na mwenye eneo hilo.

Hata hivyo Mabubu alisema kuwa,Ofisi za madini zimewapatia mamlaka makubwa viongozi wa serikali za vijiji na unapofika katika ofisi hizo kabla ya kusikilizwa anambiwa umeshafika kwa mwenyekiti wa kijiji,hali ambayo wengi waklipewa maeneo wanawaamini sana viongozi hao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live