Serikali imesema Mgodi wa Barrick North Mara unakusudia kutoa kifutajasho kwa wananchi wa kitongoji cha Namichele ambao wamepata madhila ya kusitisha matumizi ya ardhi yao ili kuruhusu shughuli za mgodi huo.
Uamuzi huo ambao umetangazwa leo Aprili 24, 2023 Bungeni jijini Dodoma unatokana na maamuzi ya Mgodi wa Barrick kusitisha nia ya kutumia eneo la kitongoji cha Nyamichele.
“Mgodi wa Barrick North Mara kwa sasa hauhitaji eneo la kitongoji cha Nyamichele kama wananchi walivyokuwa wametarajia hapo kabla. Pamoja na Mgodi wa North Mara kutohitaji eneo hilo, kuna utaratibu ambao unaandaliwa na mgodi huo wa kutoa kifutajasho kwa wananchi waliopata madhila kutoka kwa mgodi huo,” amesema Naibu Waziri wa Madini, Dk. Steven Kiruswa.
Kiruswa alikua akijibu swali na Mbunge wa Viti Maalam, Esther Matiko aliyetaka kujua ni lini Wananchi wa Kitongoji cha Nyamichele watalipwa fidia kutokana na madhila waliyoyapata kutoka Mgodi wa Barick