Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mfumuko wa bei wafikia asilimia 3.7

Mfumuko Tz Tz Mfumuko wa bei wafikia asilimia 3.7

Tue, 14 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba amesema katika mwaka 2021 mfumuko wa bei uliongezeka kwa wastani wa asillimia 3.7 ikilinganishwa na wastani wa asilimia 3.3 mwaka 2020.

Dk Mwigulu amesema hayo leo Jumanne Juni 14, 2022 wakati akiwasilisha hali ya uchumi wa Taifa na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka wa fedha 2022/23.

Amesema mfumuko wa bei umeendelea kuwa ndani ya lengo la wigo wa asilimia 3 hadi 5.

“Mfumuko wa bei ulifikia wastani wa asilimia 3.8 Aprili 2022 ikilinganishwa na asilimia 3.3 Aprili 2021.

“Kuongezeka kwa mfumuko wa bei kulichangiwa na sababu zilizo nje ya udhibiti wa Serikali zikiwemo kuvurugika kwa mnyororo wa uzalishaji na usambazaji wa bidhaa na huduma katika soko la dunia kutokana na athari za vita baina ya Urusi na Ukraine” Dk Mwigulu

Chanzo: www.tanzaniaweb.live