Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mfumuko wa bei waendelea kushuka

11122 Mfumuko+pic TanzaniaWeb

Tue, 10 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mfumuko wa bei kwa Juni 2018 umepungua hadi asilimia 3.4 ikilinganishwa na asilimia 3.6 ya Mei mwaka huu.

Mkurugenzi wa sensa ya watu na takwimu za jamii, Ephraim Kwesigabo alisema jana kuwa hali hiyo imechangiwa na kupungua kwa bei za bidhaa zisizo za vyakula.

Alibainisha kuwa bidhaa zisizo za chakula zimechangia kwa kiwango kikubwa kupungua kwa mfumuko wa bei kati ya Juni 2017 na Juni 2018.

“Bia zilipungua kwa asilimia 1.1, gharama za ukarabati wa vifaa vya umeme na viyoyozi kwa asilimia 1.8, gesi ya kupikia kwa asilimia 5.6 na majiko ya mkaa kwa asilimia 2.0,” alisema Kwesigabo.

Kuhusu mfumuko wa bei za vyakula na vinywaji baridi, Kwesigano alisema mpaka Juni uliongezeka hadi asilimia 3.4 kutoka asilimia 2.6 uliokuwapo Mei.

Wakati mfumuko ukipungua nchini, hali imekuwa tofauti kwa nchi za Afrika Mashariki.

Nchini Uganda, Kwesigabo alisema kwa mwaka ulioishia Juni mfumuko umeongezeka hadi asilimia 2.2 kutoka asilimia 1.7 uliokuwapo mwaka ulioishia Mei.

Hata Kenya, mfumuko huo umeongezeka hadi asilimia 4.28 kutoka asilimia 3.95 za mwaka ulioishia Mei.

Chanzo: mwananchi.co.tz