Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mfumuko bei ya vyakula wafikia 4.8%

Bei Ya Vyakula Mfumuko bei ya vyakula wafikia 4.8%

Wed, 12 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imesema Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba 2022 umeongezeka hadi asilimia 4.8 kutoka asilimia 4.6 kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti, 2022.

NBS imesema kuongezeka kwa mfumuko huo kumechangiwa na kuongezeka kwa mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula kwa kipindi cha mwaka ulioishia mwezi Septemba, 2022 ikilinganishwa na kipindi cha mwaka ulioishia mwezi Agosti 2022.

Baadhi ya bidhaa hizo ni pamoja na Mchele, Unga wa ngano, Unga wa mtama, Unga wa mahindi, Samaki wa maji baridi, Dagaa wakavu, Matunda, Karanga mbichi, Viazi mviringo, Maharage makavu ya kawaida, Maharage ya kombati, Soya, Njegere kavu na Kunde kavu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live