Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mfumo wa GIMIS kuleta mapinduzi katika huduma za Ununuzi wa Umma

Gpspic Data Mfumo wa GIMIS kuleta mapinduzi katika huduma za Ununuzi wa Umma

Fri, 25 Mar 2022 Chanzo: mwananchi Digital

Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) ni miongoni mwa Taasisi zinazojivunia mafanikio katika kipindi cha mwaka mmoja cha Serikali ya awamu ya sita ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuanza kutoa huduma zake kwa njia ya mfumo wa kielektroniki wa GPSA Integrated Management Information System (GIMIS).

Wakala ilianzishwa kwa mujibu wa sheria ya Wakala za Serikali Na.30 ya mwaka 1997 na mabadiliko yake, kupitia Agizo la uanzishwaji wa Wakala “The Executive Agencies Establishment Order 2007” na kutangazwa katika Gazeti la Serikali Na.235 la Desemba 7, 2007.

Aidha Agizo la uanzishwaji lilifanyiwa marekebisho tarehe 13 Aprili, 2012 kupitia Tangazo Na.133. Wakala ulizinduliwa rasmi Juni 16, 2008 na una ofi si katika mikoa yote ya Tanzania bara. Majukumu ya Wakala kwa mujibu wa Sheria ya Uanzishwaji wake ni kama yafuatavyo;

• Kutoa Huduma toshelevu ya vifaa kwa ubora na bei shindani;

• Kutoa huduma ya Ugomboaji na Uondoshaji Mizigo, na Ushauri wa Kitaalam kwa kuzingatia thamani halisi ya fedha;

• Kuandaa na Kutoa Orodha ya Wazabuni wa Vifaa na Huduma Mtambuka (VHM) kupitia Mikataba Maalum;

Advertisement • Kutoa huduma ya kuhifadhi mali na vifaa kwa kutumia maghala;

• Kuhakikisha kuwa Wakala unakuwa endelevu.

Wakala ni miongoni mwa Taasisi katika sekta ya Ununuzi wa Umma ambapo sekta hii inakadiriwa kuwa na matumizi zaidi ya asilimia 70 ya bajeti ya Serikali, hivyo basi maboresho ya utoaji wa huduma zake kidijitali ni mapinduzi makubwa katika sekta hii.

Wadau wanaotumia huduma za Wakala ni pamoja na Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala za Serikali, mashirika ya Umma, Mamlaka mbalimbali za Udhibiti, Taasisi za fedha, Bodi za Kitaaluma, Serikali Kuu, Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa na Umma kwa ujumla.

Maboresho haya ni muitikio wa Wakala kwa vitendo wa muelekeo wa Serikali ya awamu ya sita ya kutumia mifumo ya Tehama katika utoaji wa huduma za Taasisi za Umma.

Wakala umeanza kutumia rasmi mfumo wa ‘GPSA Integrated Management Information System’‑(GIMIS) mnamo Machi 1, 2022, hii ni kufuatia kukamilika kwa mfumo huu uliojengwa na Mamlaka ya Serikali Mtandao

(eGA).

Mfumo huu ni jumuishi wa huduma zinazotolewa na Wakala unaowezesha Taasisi za Umma kupata huduma kidijitali popote walipo kwa kutumia vifaa vya kielektroniki kama vile simu na kompyuta.

Mfumo umerahisisha utekelezaji na taarifa kwa Taasisi za Umma kuwezekana popote walipo ikiwemo kupata orodha ya vifaa vinavyopatikana, kupata bei ya vifaa vinavyopatikana, kupata bakaa ya amana ya Taasisi, kupata bili kwa ajili ya kufanyia malipo na kupata stakabadhi baada ya kufanya malipo.

Mfumo huu ni muhimu na una faida mbalimbali ikiwemo kusaidia kuokoa muda na kupunguza gharama za matumizi ya karatasi (paperwork), uharaka na urahisi wa upatikanaji wa taarifa zinazohifadhiwa kidijitali, na kuongeza uwajibikaji na uboreshaji wa utoaji wa huduma.

Wadau wote wa Wakala wanaendelea kukumbushwa kujisajili katika mfumo huu ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za Wakala kwa kujaza fomu zinazopatikana katika tovuti kupitia anuani ya ‘www.gpsa.go.tz’.

Chanzo: mwananchi Digital