Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mfumo mpya wa malipo kurahisisha ununuzi

Lawyer Payment Methods.png Mfumo mpya wa malipo kurahisisha ununuzi

Wed, 22 Mar 2023 Chanzo: mwanachidigital

Watanzania sasa watafanya malipo ya bidhaa na huduma kwa njia ya mtandao baada ya kamapuni za Tigo, Selcom pamoja na Mastercard kuzindua huduma ya kadi mtandao.

Akizungumza katika uzinduzi huo jana Machi 21, Ofisa mkuu wa Tigo pesa, Angelica Pesha amesema huduma ya kadi mtandao inayotambulika kama ‘Tigopesa Mastercard Virtual card’ itamrahisishia mteja kufanya malipo ya bidhaa tofauti mtandaoni akiwa nchi yoyote duniani pale ambapo mastercard inakubalika.

“Tigopesa Mastercard itasaidia kurahisisha ununuzi wa bidhaa mtandaoni, ambapo kadi mtandao hiyo itakuwa ni ya siku saba, hadi siku 90 baada ya hapo mteja anaruhusiwa kufungua nyingine bila ya kufanya malipo yoyote,” amesema.

Pesha amesema huduma hiyo ya kadi mtandao itawasaidia Watanzania na wateja wengine duniani kufanya malipo mtandaoni hata kwa wale wasio na akaunti za kibenki ambapo huongeza uchangiaji wa ajenda ya ujumuishaji wa wateja kiuchumi.

“Ili kupata huduma hiyo mteja wa tigopesa anapaswa kutengeneza kadi hiyo kupitia program tumizi ya Tigopesa (Tigopesa App) na kwa wale wanaotumia simu rununu huduma inapatikana katika mfumo wa tigopesa,” amesema

Akizungumzia masuala ya usalama baada ya mteja kufungua Tigopesa Mastercard amesema matumizi ya neno la siri ni njia pekee ya usalama, hivyo hata wafanyakazi wa tigo hawawezi kufahamu neno siri la mteja wa Mastercard.

“Katika hili mnatakiwa kutambua neno siri linalowekwa katika tigopesa mastercard lazima lifanane na lile la akaunti yako ya Tigopesa,’’ amesema

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Selcom, Sameer Hirji yeye amesema wamekuwa wakifanya kazi na Tigo kwa takribani zaidi ya miaka 10 hivyo anaamini huduma hiyo ya kadi mtandao itawarahisishia wateja kufanya miamala mtandaoni ambapo mtu atakuwa na uwezo wa kulipia huduma kama Netflix.

Naye, mwakilishi wa Mastercard, Lenin Oyuga ameeleza kwamba, anaamini katika ushirikiano ambao unachagiza maendeleo mbalimbali katika jamii zetu.

“Tigopesa mastercard inasaidia watumiaji wa tigo kununua aina yoyote ya bidhaa mtandaoni, kwa kuwa ubunifu wetu unalenga katika kuboresha mabadiliko ya kidijitali,” amesema

Chanzo: mwanachidigital