Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mfumo mpya kutumika Soko la Hisa DSM

Hisa Dar Morami Marwa, Mkurugenzi Mtendaji DSE

Wed, 4 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Soko la kuu la hisa la Dar es Salaam, limetangaza mfumo mpya utakao wawezesha wafanyabiashra wadogo na wakati kuweza kupata ufadhili wa muda mrefu wa kifedha kutoka kwa wawekezaji .

Kupitia mradi walioupa jina la "endeleza project" wafanyabiashara hao watapata mafunzo wezeshi ya biashara kwa ajili ya kujenga biashara imara.

Mkurugenzi Mtendaji wa Soko la Hisa la Dar es Salaam Morami Marwa, amesema kuwa mpangiohuu utamaliza tatizo la upatikanaji wa mikopo ya muda mrefu linayowakabili wafanyabiashara hao

"Kupitia mradi huu, wafanyabiashara waliopitishwa watapokea mafunzo juu ya kitaaluma kuhusu upangaji wa taarifa za kibiashara, jinsi ya kupanga taarifa za mapato na matumizi ya pesa, usimamizi wa biashara kwa ujumla"

Aliongeza kusema kuwa mradi huo sio sehemu ya biashara ya soko la hisa ila una lengo la kukuza biashara hizo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live