Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mfuko wa Ma-Hustler umetoa Sh.Bil 7.77 mikopo kwa machinga

 119966349 Ejfwaefxgai 17v Mfuko wa Ma-Hustler umetoa Sh.Bil 7.77 mikopo kwa machinga

Fri, 2 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jumla ya Sh milioni 408 za Kenya ama Sh bilioni 7.77 za Tanzania zimetolewa ndani ya saa 24 tu baada ya kuzinduliwa kwa Mfuko wa Hustler, Mpango maalumu unaowawezesha vijana na machinga kukopa bila riba.

Katibu wa Baraza la Mawaziri la Vyama vya Ushirika na MSMEs Simon Chelugui amesema kuwa Wakenya milioni 1.14 tayari wamenufaika na mpango huo uliozinduliwa na Mpambanaji Mkuu ‘Chief Hustler’ Dk William Ruto.

Mfuko huo umeundwa mahususi kusaidia wafanyabiashara wadogo nchini.

Rais William Ruto alizindua hazina hiyo iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu Jumatano akitimiza ahadi yake ya uchaguzi ya kutenga Sh bilioni 50 kwa ajili ya wapambanaji ‘ma-hustler.'

"Kupitia uzinduzi wa hazina hii, tunasaidia Wakenya wasio na uwezo wa kutosha kwa huduma na bidhaa na vile vile kuwakomboa kutoka kwa machafuko na kuanzisha utamaduni wa kuweka akiba, uwekezaji na usalama wa kijamii," Ruto alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live