Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

'Mfuko mmoja wa cement tofali 30' Mkuu maabara ya Ujenzi TBS

Download 8.jpeg 'Mfuko mmoja wa cement tofali 30'

Sat, 19 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wazalishaji wa matofali ya saruji wametakiwa kuzalisha matofali ambayo yanakidhi viwango vya ubora ili kuepuka madhara makubwa yatakayojitokeza kwa mtumiaji.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Maabara ya Ujenzi TBS, Mhandisi Mahona William mara baada ya waandishi wa habari kufanya ziara katika maabara za Shirika la Viwango Tanzania jana tarehe 18/03/2022 Jijini Dar es Salaam.

Amesema tofali linatakiwa liwe limegandamizwa mchanga wa kutosha ambao utafanya tofali liwe imara na lenye kukidhi viwango vinavyotakiwa.

“Tunashauri kwa ujenzi wa kawaida angalau mfuko mmoja wa saruji uweze kutoa tofali 30 ambazo zitakuwa zinakidhi viwango vinavyotakiwa” Mkuu wa Maabara ya Ujenzi TBS

Waandishi wa habari wamefanya ziara hiyo kujifunza na kujionea mabara za TBS zinavyotekeleza majukumu yake katika kupima sampuli.

MBOWE AFUNGUKA “NITACHUKUA MAKOMANDOO, WADOGO LAKINI BALAAH, NAWAHITAJI MAKOMANDOO”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live