Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mfanyabiashara maarufu mjini Moshi achunguzwa

44175 Swai+pic Mfanyabiashara maarufu mjini Moshi achunguzwa

Thu, 28 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Moshi. Vyombo vya uchunguzi ikiwamo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) vimevamia biashara za mfanyabiashara tajiri wa Moshi, Vicent Laswai vikimchunguza kwa tuhuma za ukwepaji kodi.

Biashara zake yakiwamo maghala matatu ya kuhifadhi bidhaa mbalimbali kutoka nchini Kenya yaliyopo maeneo mbalimbali ya mji wa Moshi na duka la jumla vimewekwa chini ya uchunguzi wa vyombo hivyo

Laswai mwenyewe jana na juzi hakupatikana kueleza juu ya uchunguzi huo kutokana na simu yake kutokuwa hewani na marafiki wa karibu wanadai yuko nchini India kwa matibabu.

Uchunguzi huu mpya unakuja ikiwa ni mwezi mmoja tu umepita, tangu Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuamuru kufungwa kwa duka lake kubwa la kubadilisha fedha la Trast lililopo mjini Moshi

Kufungwa kwa duka hilo nako kulikuja miezi mitatu baada ya BoT kufunga maduka 30 ya kubadilisha fedha jijini Arusha likiwamo la Central Forex ambalo lilikuwa ni tawi la duka lake la Trast la Moshi.

Operesheni hiyo iliyohusisha pia polisi lakini Kamanda wa Polisi mkoa Kilimanjaro, Hamis Issah hakupatikana ofisini na hata alipopigiwa simu yake ya mkononi hakupokea ingawa juzi alionekana akiwa na kikosi kazi hicho majengo ya TRA.

Mkurugenzi wa huduma na elimu kwa mlipa kodi wa TRA, Richard Kayombo alithibitisha kuwapo kwa uchunguzi huo, lakini akakataa kueleza chochote akisema itakuwa ni kuingilia uchunguzi.



Chanzo: mwananchi.co.tz