Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mfahamu zaidi Mfanyabiashara Tanil Somaiya.

Somaiya Mfanyabiashara wa Kitanzania Tanil Somaiya

Mon, 16 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mfanyabiashara wa Kitanzania Tanil Somaiya ambaye alifariki siku ya jumatano ya tarehe 11/08/2021, unaweza kusema aliishi kwa ukimya enzi za uhai wake bila umaarufu wowote, kwa muongo 1. Takwimu zinaonyesha kuwa maisha yake katika biashara yalikumbana na misukosuko mingi.

Kutoka kwenye kuuza Vocha za sh 500 kwenye kampuni za mawasiliano pia Bwn. Somaiya alijiingiza kwenye kashfa kubwa ya rada za jeshi na Mikataba ya ndege za Rais.

Bwa. Somaiya ambaye ni mwanzilishinwa wa Kampuni ya Shivacom ambayo ilifanya kazi zaidi miaka ya 2000 alizaliwa 8 octoba 1968.

Baada ya kampuni hiyo kushinda tenda ya kusambaza vocha miaka 10 iliyopita wengi wanaweza kuona ni namna gani alikuwa mfanyabaishara mkubwa na umahiri aliotumia katika kukamilisha mpango huo wa suala la vocha.

Baada ya miaka kdhaa kamati ya bunge Viwanda na Biashara ilifanya uchunguzi wa kampuni yake kwa kuuza vocha za Vodacom ambazo tayari zimekwisha kutumika.

Ingawa haikujulikana kwa undani juu ya matokeo ya uchunguzi, ambayo yalileta etieti kwa jamii, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) ilidai kupoteza mabilioni ya mapato kwa mfanyabiashara huyo.

Kampuni ya Shivacom ya Bwn. Somaiya kitaalamu ilijikita katika kuwekeza kwenye usambazaji wa Radio za Motorola na alikuwa ni Mhandisi wa kwanza aliyekuwa na utalaamu kwenye magari na kwenye program ya mifumo ya usalama.

Licha ya kwamba maisha yake binafsi ya tajiri huyu hayafahamiki kwenye jamii, kinachojulikana zaidi ni kwamba alipata umaarufu baada ya kuanza kuchunguzwa dhidi ya madai ya kuhusika kwake kwenye mikataba kadhaa ya jeshi pamoja na kuuzia jeshi rada zenye thamani zaidi Dola milioni 40 kutoka kampuni ya Uingereza katika kipindi cha Utawala wa Hayati Rais Benjamini Mkapa.

Katika kesi yake ya Mifumo ya udhibiti wa Anga (radar) Bwn. Somaiya alijikuta ameingia kwenye orodha ya wabadhirifu, orodha ambayo ilikuwa ikitolewa na Uingereza kupitia kampuni ya SFO mwezi january mwaka 2007 baada ya Uingereza kukubali kuchukua jukumu la kuwabaini mafisadi na wala rushwa ulimwenguni na Tanzania ikiwemo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live