Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mfahamu tajiri namba moja duniani, Bernard Arnault

Bilionea Namba Moja Dunian.jpeg Mfahamu tajiri namba moja duniani, Bernard Arnault

Thu, 15 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bernard Arnault, mwenyekiti wa kampuni kubwa ya mitindo Ufaransa ya bidhaa za kifahari LVMH (Louis Vuitton Moët Hennessy) amekuwa mtu wa kwanza kutoka Ulaya kuongoza orodha ya Bloomberg ya watu matajiri zaidi duniani akimshusha Elon Musk hadi nafasi ya pili.

Utajiri wa Arnault umefika dola bilioni 171 [TZS trilioni 400] ukimshusha Musk hadi namba mbili, huku thamani ya Musk ikitajwa hivi karibuni kuwa $164 bilioni [TZS trilioni 383] kulingana na Bloomberg Billionaires Index. Arnault tayari alikuwa amemwondoa Musk kutoka nafasi ya juu kwenye orodha ya Forbes ya “Real Time Billionaires” wiki iliyopita.

Thamani ya Musk imeshuka kwa dola bilioni 107 [TZS trilioni 250] mwaka huu, kulingana na Bloomberg.

Ununuzi wa Musk wa Twitter haujasaidia pia. Japo kuwa bado hayuko katika hatari ya kuporomoka zaidi kwenye orodha, utajiri wake ukiwa mkubwa zaidi kuliko raia wa India, Gautam Adani ($125 billion) na mwanzilishi wa Amazon, Jeff Bezos ($116 billion).

Bei ya hisa za Tesla (TSLA) imeshuka kwa asilimia 54 mwaka huu, wakati hisa za LVMH zikipanda baada ya mauzo ya juu nchini Marekani na Ulaya. LVMH ina thamani ya soko ya $386 bilioni [TZS trilioni 900].

Mzaliwa wa Roubaix, Kaskazini mwa Ufaransa mnamo 1949, Arnault alihitimu kutoka shule ya kifahari ya École Polytechnique, shule ya uhandisi huko Paris. Alianza kazi yake katika kampuni ya ujenzi inayomilikiwa na familia, Ferret-Savinel, na kuwa mwenyekiti mnamo 1978 baada ya kupandishwa vyeo mfululizo.

Arnault alinunua kiasi kikubwa cha hisa za LVMH mnamo 1989, miaka miwili baada ya kampuni kuundwa kwa muunganisho wa Louis Vuitton na Moët Hennessy. Amekuwa mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni tangu wakati huo.

Bilione huyo ameoa na ana watoto watano, ambao wote kwa sasa wanafanya kazi katika LVMH au moja ya chapa zake, kulingana na Bloomberg.mfahamu

Chanzo: www.tanzaniaweb.live