Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mfahamu Mompha Junior, Bilionea Mtoto Mwenye Umri wa Miaka 9

Muhammed Awal Mustapha.jpeg Mfahamu Mompha Junior, Bilionea Mtoto Mwenye Umri wa Miaka 9

Wed, 2 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mfahamu, Muhammed Awal Mustapha maarufu kama Mompha Junior mtoto mwenye umri wa miaka tisa (9), ambaye ni miongoni mwa mabilionea wenyeumri mdogo zaidi duniani.

Mompha Junior ni mtoto wa kiume wa mmiliki wa kampuni kubwa ya intaneti ya Nigeria Ismailia Mustafa, ambaye pia anafahamika kwa jina Mompha.

Mvulana kijana huyu alipewa nyumba yake ya kwanza akiwa na umri wa miaka 6.

Mompha Junior, mara kwa mara hutuma picha zake nzuri kwenye mtandao wake wa kijamii wa Instagram, akionyesha mtindo wake wa maisha ya kifahari.

Awali aliushirikisha umma picha ya ndege yake aina ya jet, ambapo akiandika “Usimdharau yeyote bure, na fanya kazi kwa bidii. Mungu awabariki watu .”

Baba yake Willkan Bw Mompha, ambaye ni meneja mkuu wa kituo cha kubadili pesa-Lagos Bureau De Change, anashutumiwa kwa ubadhilifu wa pesa wa zaidi ya dola milioni 10.

Mapema mwezi huu, mahakama ya Nigeria ilisikiliza kesi iliyowasilishwa na tume ya Nigeria ya kupambana na ufisadi dhidi ya Bw Ismail, iliyodai kuwa alikuwa amefanya ubadhilifu wa pesa kutoka katika biashara yake ya nyumba, ingawa Bw Ismael anakanusha madai hayo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live