Meta ambayo ni Kampuni mama ya Facebook na Instagram imekifunga kituo chake cha Afrika Mashariki kinachohusika na kudhibiti na kuhakiki maudhui kilichopo jijini Nairobi.
Tetesi zinaeleza kuwa uamuzi huo unatokana na mshiriki wao kibiashara ambayo ni Kampuni ya Sama kuamua kusitisha huduma ya udhibiti na uhakiki wa maudhui yenye madhara (harmful content).
Taarifa kutoka Nairobi zinasema kuwa kufikia mwezi Machi shughuli zote za mwisho pamoja na makabidhiano yatakuwa yamekamilika.
Hatua hiyo itasababisha takribani watu 200 kupoteza ajira na wengine wengi ambao ni raia wa kigeni kubaki bila vibali vya kufanyia kazi.