Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Meli zenye usajili wa Tanzania zaagizwa kuajiri wazawa

Meliipic Data Meli zenye usajili wa Tanzania zaagizwa kuajiri wazawa

Sat, 25 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imeziagiza meli zote zilizosajiliwa nchini na zinazopeperusha bendera ya Tanzania kutoa fursa za ajira kwa mabaharia Watanzania.

Agizo hili limetolewa Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, MWasiliano na Uchukuzi Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Amour Hamil Bakar wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Bukoba yanakofanyika maadhimisho ya siku ya mabaharia.

“Serikali zetu mbili za Bara na Visiwani zitasimamia utaratibu mzuri utakaohakikisha na kusimamia maslahi ya mabaharia ikiwemo kukatiwa bima itakayowahakikishia malipo ya fidia wanapokumbwa na majanga kazini," amesema Bakar

Amesema Serikali itashirikisha taasisi na wadau wengine wa sekta ya usafirishaji majini katika kazi kusimamia utekelezaji wa sheria zinazolinda haki na maslahi ya mabaharia kutokana na umuhimu wa kada hiyo kwenye masuala ya majini.

Awali akizungumza kwa niaba ya Chama cha Mabaharia Tanzania Bara (Tasu), Katibu Mkuu wa Chama cha Mabaharia Zanzibar (Zasu), Hussein Nassor Uki ametaja ukosefu wa ajira kwenye meli za nje zinazosajiliwa nchini na kupeperusha bendera ya Tanzania na mazingira magumu ya kazi kwa mabaharia wanawake kuwa miongoni mwa changamoto zinazowakabili mabaharia nchini.

"Mabaharia wanawake nao wanakabiliwa na mazingira magumu ya kazi melini kutokana na kukosekana kwa vyumba maalum vya faragha wawapo kazini," amesema Uki

Advertisement Amesema mabaharia Watanzania pia hawapewi kipaumbele katika fursa za ajira kwenye meli za utafutaji, uchimbaji na usafirishaji wa mafuta au gesi zinazofanya kazi nchini.

"Baadhi ya mabaharia pia hufanya kazi bila kuwa na mikataba huku wakilipwa viwango vidogo vya mishahara. Hii inasababishwa na kukosekana kwa elimu ya sheria za kazi na usalama wa mabaharia nchini," amesema Uki

Amesema changamoto hiyo inachangiwa na ushirikiano mdogo wa wamiliki wa vyombo usafirishaji majini kwa vyama vya mabaharia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live