Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Meli ya mizigo kuto Kenya yageuka kivutio Mwanza

MV Uhuru 860x573 Meli ya mizigo kuto Kenya yageuka kivutio Mwanza

Thu, 2 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MELI kubwa ya mizigo ya Mv. Uhuru 1 kutoka Kisumu nchini Kenya imetia nanga katika Bandari ya Mwanza Kusini ikiwa na mabehewa 21 yenye jumla ya tani 771 yakiwa na shehena ya saruji huku ikielezwa kuwa ni takribani miaka kumi imepita tangu meli hiyo ya mizigo ifike katika bandari za Ziwa Victoria.

Meneja wa bandari za Ziwa Victoria (TPA) Erasto Jackson amesema kuwa kwa sasa Mamlaka ya bandari nchini ipo katika maboresho makubwa ya bandari zake ndani ya ziwa Victoria.

Kwa upande wake Josephat Rono ambaye ni mfanyabiashara na mmiliki wa mzigo huo amesema kuwa ameamua kutumia meli hiyo ya Mv. Uhuru 1 ikiwa ni sehemu ya kupunguza gharama za kusafirisha mzigo,huku akitoa pongezi kwa Mamlaka ya bandari nchini kwa mapokezi mazuri aliyopata. -

Chanzo: www.tanzaniaweb.live