Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Meli ya mafuta ya kula yamaliza kupakua

62362669e48d5f106e40150fb14db4cd Meli ya mafuta ya kula yamaliza kupakua

Wed, 20 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

UHABA wa Mafuta ya kula nchini na kupanda kwa bei yake kutaanza kupungua ndani ya siku chache kuanzia sasa, baada ya tani zaidi ya 26,500 za mafuta hayo kuingia Januari 16 mwaka huu na jana usiku meli yenye shehena hiyo imemaliza kupakua mafuta hayo katika Bandari ya Dar es Salaam.

Akizungumzia shehena hiyo jana katika Kituo cha Mita za Kupima Mafuta cha Kurasini (KOJ), Kaimu Meneja wa Kituo cha Mafuta wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Sixtus Kavia, alisema walipokea meli iitwayo Melitasat Januari 16,2021 ikiwa na shehena ya mafuta zikiwemo tani 26,500 za mafuta ya kula.

Alisema mafuta hayo yameagizwa na kampuni na viwanda mbalimbali vya ndani vinavyoagiza na kusambaza mafuta hayo na kwamba hadi jana walikuwa wameshashusha tani 10,000 na jana hiyo hiyo usiku walitegemea shehena yote iwe imeshapakuliwa.

“Meli ya mafuta hiyo hapo inaendelea kushusha shehena za matufa ya kula, na hadi leo usiku(jana), tunategemea shehena yote tani 26,500 ziwe zimeshashushwa na tayari wameshaanza kusambaza hivyo uhaba wa mafuta hayo utapungua’’alisema Kavia.

Akizungumzia hilo, Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Elihuruma Lema alisema bei ya mafuta ya kula imepanda sio tu kwa sababu ya kuadimika kwa bidhaa hiyo,bali ni kutokana na bei ya mafuta katika soko la dunia kupanda kutokana na baadhi ya viwanda na wazalishaji kusimama kwa sababu ya mlipuko wa corona.

Lema alisema saa baadhi ya viwanda na wazalishaji wameanza tena kazi na kuwa kwa mwezi mmoja bandari ya Dar es Salaam hupokea meli moja au mbili za mafuta ya kula na kwamba Januari 3, mwaka huu meli iitwayo MT.UACC SHAMIYA iliyoleta shehena ya mafuta ya kula ilimaliza kupakua na kuondoa.

“Kwa wastani bandari ya Dar es Salaam tunapokea meli moja au mbili kwa mwezi zinazoleta mafuta ya kula nchini na hadi sasa tangu kuanza kwa sakata la mafuta hayo kupanda bei na kuadimika, tumeshapokea meli mbili, imani yetu ni kwamba waagizaji na wasambazaji wanaendelea kuyasambaza ili kupunguza uhaba uliokuwepo’’alisema Lema.

Wiki chache zilizopita, Waziri wa Viwanda na Biashara, Geoffrey Mwambe aliwahakikishia wananchi kuwa hali ya upatikanaji wa mafuta ya kula itatengemaa mara baada meli mbili za mafuta hayo kuwasili nchini.

Chanzo: habarileo.co.tz