Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Meli ya kifahari kufanya 'Royal Tour' na watalii 715

Meli Kifahariiiii Meli ya kifahari kufanya 'Royal Tour' na watalii 715

Tue, 18 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meli ya kitalii ya Seabourn Sojourn imewasili nchini Tanzania leo Aprili 17 na watalii 715 ikiwa ni mkakati maalum wa kuhakikisha Tanzania inavuka lengo la idadi ya watalii milioni tano ifikapo mwaka 2025.

Akizungumzia ujio wa meli hiyo, Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Lily Fungamtama amesema ujio wa meli hiyo ni ushahidi tosha kuwa Filamu ya Royal Tour imeitangaza Tanzania Kimataifa huku akisizitiza kuwa meli nyingi zaidi za watalii zinatarajiwa kuja siku za usoni.

Amesema watalii hao mara baada ya kuwasili katika Bandari ya Dar es salaam wamepata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ya Jiji ikiwemo Makumbusho ya Taifa, Kijiji cha Makumbusho, soko la vinyago lililoko Mwenge na viwanja vya Mnazi Mmoja na kuitaja Tanzania kama nchi yenye fursa nyingi za utalii.

Meli hiyo ilianza safari yake kutoka nchini Marekani ikiwa na raia wa mataifa mbalimbali ya Ulaya imetia nanga katika bandari ya Dar es Salaam ikitokea Zanzibar baada ya hapo itaelekea nchini Afrika Kusini.

Aidha, Watalii wengine mara baada ya kuwasili nchini wamepata fursa ya kwenda kutembelea Hifadhi za Taifa ya Serengeti na Ngorongoro.

Mmoja wa watalii hao, Burton Nadiolado amesema kuwa ilikuwa ndoto yake kubwa kutembelea barani Afrika na hatimaye amefika Tanzania nchi inayosifiwa kwa ukarimu

Chanzo: www.tanzaniaweb.live