Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Meli ya abiria Comoro- Mtwara yaanza kazi

Meli Mtwara Mtwaraa.png Meli ya abiria Comoro- Mtwara yaanza kazi

Fri, 19 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

CHEMBA ya Wafanyabiashara Wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA) kwa kushirikiana na muwekezaji kutoka visiwa vya Commoro wamezindua meli ya abiria itakayofanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Mtwara.

Meli hiyo imezinduliwa leo Aprili 19, 2024, mara baada ya kuwasili Bandari ya Mtwara ikitokea Comoro kuleta abiria wakiwemo watu wanaokuja kwa ajili ya matibabu katika Hispotali ya Taifa Muhimbili na Hospital ya Rufaa kKanda ya Kusini.

Akizungumza katika uzindizi wa meli hiyo ya kwanza ya abiria tangu kufanyika uboreshaji wa Bandari, Makamu wa Rais wa TCCIA Swallah Said Swallah, amesema meli hiyo ina uwezo wa kubeba abiria 300 na mizigo mchanganyiko wa vyakula tani 150.

Mali hiyo inatarajiwa kufanya safari zake mara mbili kwa mwezi ikileta abiria kutoka Comoro hadi Mtwara na kutoka Mtwara kwenda Comoro ikipeleka pia mazao ya biashara. - Amewataka wafanyabiara wa Mtwara kuchangamkia fursa ya kupeleka bidhaa za biashara hususan vyakula na mazao yote yanayolimwa kwenye Mikoa ya Lindi, Ruvuma na Mtwara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live