Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Meli ya Uhispania yatua na tani 50 za samaki

Meli Uhispania Uhispania (600 X 342) Meli ya Uhispania yatua na tani 50 za samaki

Fri, 24 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WAZIRI wa mifugo na uvuvi, Abdallah Ulega amepokea tani 50 za samaki wasiolengwa "bycatch" Kutoka kampuni ya Albacora ya Nchini Uhispania inayofanya kazi kwenye bahari kuu kupitia meli kubwa ya uvuvi inayojulikana kama Pacific Star.

Mapokezi hayo yamefanyika leo katika Bandari ya Dar es Salaam wakati wa ukaguzi wa meli hiyo ikiwa ni makubaliano ya pande mbili za nchi hizo kuhakikisha samaki wanapovuliwa wasiotarajiwa wanarudishwa nchi husika.

“Baada ya ushawishi mkubwa kampuni hiyo Imeridhia kuwekeza Tanzania badala ya kuchukua samaki kwenda kuchakata nchini Kwao basi watachakata hapahapa na mpaka sasa wameshanunua ardhi mkoani Tanga Ili kuanzisha kiwanda cha uchakataji wa samaki,” amesema Ulega.

Amesema baada ya kushushwa kwa samaki hao itasaidia kushuka kwa bei ya samaki kwenye masoko mbalimbali likiwemo Soko la Ferry Ulega.

"Matarajio yetu watatoa ajira zisizopungua 100 kwa vijana wa kike na wakiume wa Tanzania, kwa sasa hivi kuna mabaharia wengi lakini miongoni mwa mabaharia hao ni vijana wa kitanzania. Tunaendelea kuwapa uzoefu, na leo wanashuka vijana wawili kutoka Zanzibar na wanaopanda kutoka Tanzania bara ili kutoa nafasi kwa vijana wote wa kitanzania." Amesema waziri huyo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo amesema zaidi ya tani 50 zitaenda kupunguza gharama ya samaki sambamba na kujifunza uvuaji wa samaki bila kutumia uvuvi ulio haramu. -

Chanzo: www.tanzaniaweb.live