Waziri wa Uvuvi na Mifugo Abdalah Ulega amesema katika bandari ya uvuvi Kilwa Masoko mkoani Lindi kutakuwa na karakana ambayo itatumika kutengeneza meli.
Waziri Ulega ameyasema hayo mkoani Lindi katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa bandari ya uvuvi wilayani Kilwa.
Amesema katika bandari hiyo pia kutakuwa na sehemu ya maegesho ya meli kubwa kutoka maeneo mbalimbali duniani kwa wakati mmoja zenye urefu wa mita 30.
Pia kutakuwa na karakana ya kutengeneza nyavu kwa mikono na kuunganisha, na bandari hiyo itakuwa na uwezo wa kuchukua mashua, boti ndogo na mitumbwi isyopungua 200 ambayo itaegeshwa katika bandari hiyo ya uvuvi Kilwa Masoko.